History & cultureBaharia TVRC MALIMA AWA MBOGO, AJIAPIZA KUMRUDISHA DED KWA WAZIRI WAKE SHEMDOE

RC MALIMA AWA MBOGO, AJIAPIZA KUMRUDISHA DED KWA WAZIRI WAKE SHEMDOE

Long-form7:57News & PoliticsPublished Oct 19, 2026, 7:28 AM · 1d ago
Views
40
+0 views/hour
Views / hour now
0
measured 9m ago
Peak views / hour
8
8h ago
First 24 hours
40
views at 24 h
Engagement
0.0%
likes + comments / views
Likes
0
0.0% of views
Comments
0
0.00% of views
Est. ad revenue
$0–$0
lifetime, $4–9 RPM

Checked every 30 min while the video is this age · last check 9m ago · next in 20 min. YouTube itself updates public counts with a short delay.

Avg views / day
38
since upload
vs channel median
0.2×
this video's views ÷ the channel's usual
Rank in channel
#19
of 20 tracked

Views over time

20 readings

Total views Views gained per hour

Description

​Mara baada ya kufanyika kwa mnada wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Kighoma Ali Malima, amekutana na Bodi ya Usimamizi ya chama hicho, Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele, pamoja na watendaji kutoka Halmashauri za Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale, kujadili mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao la korosho mkoani humo. ​Katika kikao hicho, Mhe. Malima amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha asilimia 20 ya mapato yanayotokana na mauzo ya zao la korosho yanaelekezwa katika ununuzi na ugawaji wa miche ya korosho kwa wakulima, ili kuongeza maeneo yanayolimwa na kuongeza uzalishaji wa zao hilo. ​“Ndio hela nakwambia, Mkurugenzi, ile asilimia 20 umeifanyia kazi gani? Tumekupatia hela, hujalima hata hekari moja. Nunua miche ya korosho, igawe bure kwa wakulima. Kama nisipoona taarifa hiyo, nitakuondoa,” amesema Mhe. Malima, akisisitiza uwajibikaji katika matumizi ya fedha hizo. ​Aidha, ameitaka RUNALI kuandaa mpango mkakati madhubuti wa kusimamia na kuongeza uzalishaji wa korosho, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya chama hicho, halmashauri na taasisi za utafiti ili kuhakikisha wakulima wanapata miche bora kwa wakati. ​Sambamba na hilo, ameitaka TARI Naliendele kuimarisha juhudi za uzalishaji wa miche ya korosho kwa kuanzisha na kuendeleza vitalu vya miche, akieleza kuwa Mkoa wa Lindi uko tayari kutenga maeneo kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo. ​“Mwenyekiti, nakuamini. Nimefanya tathmini yote, nakuamini na katibu wako namwamini. Hawa TARI Naliendele wapo kilomita chache tu, watengeneze vitalu. Kila halmashauri tutatenga hekari 500 kwa ajili ya vitalu; TARI tutawapa hekari 2,000 mkoa mzima,” amesema Mhe. Malima. ​Hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa miche ya korosho, kupanua maeneo ya kilimo, kuongeza uzalishaji na kuimarisha kipato cha wakulima, pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Lindi kupitia zao hilo la kimkakati. #BahariaNews

Statistics from the YouTube Data API, tracked by FameX. Views per hour, revenue and comparisons are FameX estimates.